Klopp aomba muda wa kuisuka Liverpool | Michezo | DW | 12.10.2015
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Klopp aomba muda wa kuisuka Liverpool

Bila shaka wachezaji na mashabiki sio tu a Liverpool bali wa kandanda kwa ujumla, wanasubiri kwa hamu kumwona Jurgen Klopp akianza kazi kama kocha mpya wa Liverpool

Na kuzindua aina inayotambulika ya kandanda msimu huu ndicho kitu pekee ambacho wamiliki wa Liverpool wamemwekea Klopp.

Klopp alizinduliwa Ijumaa iliyopita kama mrithi wa Brendan Rodgers na akazusha msisimko kwa kusema kuwa anaweza kushinda taji la Premier League katika kipindi cha miaka minne ijayo lakini, katika mahojiano na gazeti la Ujerumani la Michezo Bild mwishoni mwa wiki, ameomba utulivu kwa sababu ya changamoto kubwa inayomkodolea macho. "Sasa tunastahili kuanza na siyo kusubiri. Nataka kuona hatua ya kwanza wiki ijayo na nyinyi mnataka kuona wiki ijayo lakini siyo kila mara kulinganisha na wakati mwingine. Hii ni klabu kubwa na timu nzuri, uwezo mkubwa, wachezaji wenye kasi, wachezaji wenye nguvu, walinzi wazuri, wepesi, wabunifu, kila kitu kipo. Hivyo tujaribu kuanza upya. Nadhani huu ndio wakati mwafaka wa kufanya hivyo kwa sababu kila kitu sasa ni tofauti".

Klopp alisaini mktaba wa miaka mitatu na amesema Fenway Sports Group wanaomiliki klabu ya Liverpool hawatarajii ashinde Kombe lolote au kufuzu katika Champions League katika msimu wake wa kwanza. "Sio muhimu wanachofikiria watu wakati unapoanza kazi. Ni muhimu zaidi wachofikiria watu wakati ukiondoka. Na tafadhali tupe nafasi ya kulifanyia hilo kazi. Tumejiandaa kulifanyia kazi hilo. Tunaweza kuanza katika ligi hii ambayo ni ngumu sana. Kuan wapinzani wakubwa sana lakini kwa kuzingatia mbinu ya Liverpool, tunaweza kufanikiwa. Lakini bila shaka tutayasubiri mafanikio hayo. Sitaki kusema tunaweza kusubiri kwa miaka 20 ijayo. Najua kama ntakuwa nimekaa hapa miaka minne ijayo tutakuwa tumeshinda taji moja. Hilo nina uhakika".

Mchuano wa kwanza wa Klopp kama kocha wa Liverpool utakuwa Jumamosi ijayo dhidi ya Tottenham Hotspur.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/DPA/AP/Reuters
Mhariri: Iddi Ssessanga