Klopp amwonya Guardiola kuhusu Ligi ya Premier | Michezo | DW | 11.01.2016
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Michezo

Klopp amwonya Guardiola kuhusu Ligi ya Premier

Kocha wa Liverpool Jürgen Klopp amemwonya Kocha wa Bayern Munich Pep Guardiola kuhusu msongamano wa orodha ya michuano ya Ligi Kuu ya Kandanda ya Premier nchini England

Guardiola anasemekana kuwa tayari kujiunda na Manchester City tangu kocha huyo wa zamani wa Barcelona alipothibitisha kuwa anaondoka Bayern mwishoni mwa msimu huu na anaelekea England.

Timu hiyo ya Ujerumani inaendeleana mapumziko ya msimu wa kipupwe na haijacheza mchuano wowote wa ushindani tangu Decemba 19. Liverpool itakuwa imecheza michuano tisa katika kipindi hicho wakati mabingwa hao wa Ujerumani watarejea majukumu la ligi mnamo Januari 22.

Klopp anasema kila kitu England, ni kandanda, kandanda, kandanda. Ukiwa na maandalizi mazuri ya kabla ya kuanza msimu, unakuwa na safari ndefu ndefu sana. Nnachoweza kusema kuhusu Uingerea ni uwe na matumaini, ni nchi nzuri, watu wazuri, chakula ni kizuri sana kuliko ilivyosemwa na kila mtu. Lakini hali ya hewa sio nzuri kama ilivyosema na kila mtu!. Liverpool itaialika Arsenal Jumatano, na kisha mahasimu wao wakali Manchester United Jumapili.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/DPA
Mhariri: Mohamed Khelef

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com