Klopp alalamikia VAR Premier League | Michezo | DW | 21.10.2019
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Klopp alalamikia VAR Premier League

Juergen Klopp alalamikia  VAR kuwa  haitumiki inavyostahili , baada ya  pambano la Manchester United  na  Liverpool,

Katika  ligi  ya  England, Premier League, Manchester United  jana ilifikisha  mwisho mwanzo  mzuri wa  Liverpool  wa  asilimia  100 katika  ligi  hiyo , pamoja  na  mfululizo  wa  ushindi  wa  michezo 17, kwa  kutoka  sare  ya  bao 1-1  uwanjani Old Trafford jana  Jumapili.

Hata  hivyo  ulikuwa  mchezo  mwingine  katika  Premier League uliokuwa  na  utata wa  VAR, hali itakayoendelea  kuchochea mijadala  juu  ya  mfumo  huo  ulioanza  kutumika  msimu  huu.

UEFA Super Cup - Liverpool vs Chelsea (Reuters/M. Sezer)

Kocha wa Liverpool ya Uingereza Juergen Klopp

Matokeo  hayo  yanapunguza  uongozi wa  Liverpool dhidi  ya  timu iliyoko nafasi ya  pili Manchester City hadi  pointi sita na  kikosi  cha Juergen Klopp hakikuwa  katika  hali  yake  bora. Lakini  kocha huyo wa Liverpool Juergen Klopp  analalamikia  uamuzi  wa  refa  pamoja  na VAR, baada  ya  Marcus Rashford kupachika  bao mnamo dakika  ya 36 ya  mchezo..

"Sina hakika  kama  atakiri, lakini refa Martin Atkinson , mliona mara tu, alianza  kukimbia  na  aliona kuwa litakuwa  goli. Na wakafunga na haraka akaonesha  VAR. Kwa  hiyo wasaidizi wangu  walikuwa tayari wamesimama, na kusema , tulieni. VAR inachunguza. Na nilikuwa  na  hakika ya  asilimia  100 kwamba  VAR italikataa. lakini kwa  sasa  bila  shaka  tunamatatizo. Kwa  hiyo refa  aliuacha mpira uendelee kwa  kuwa  ana  VAR, lakini VAR inasema hakuna  hakika, kwa hiyo sio faulo kwa  hiyo siwezi kulikataa."