1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Klitschko vs Fury sehemu ya pili

29 Aprili 2016

Bingwa wa zamani duniani wa heavyweight bondia Vladmir Kiltschko ameelezea matumaini kuwa atayanyakua tena mataji aliyopoteza kwa Muingereza Tyson Fury wakati watakutana katika pigano la marudiano mwezi Julai.

https://p.dw.com/p/1IfU7
Klitschko versus Fury
Picha: Reuters

Akizungumza mjini Cologne, hapa Ujerumani, Klitschko alisema pigano hilo litavutia kuanzia kengele ya kwanza hadi mwisho wake. "Yapo mengi ya kujifunza hivyo haupaswi kuacha. Hata na miaka 40, unaendelea kujifunza na kitu kinatokea ambacho sikuwa nimekipangia, kusimama hapa bila mikanda. Hivyo basi natamani sana kupambana tena mara ya pili. Tunaweza kusema mengi na kuwafurahisha watu lakini nasubiri mchuano wetu na ni kitu ambacho kinanisisimua sana na wewe pia".

Bingwa huyo wa zamani mzaliwa wa Ukraine, wa mataji ya IBF, WBA na WBO, ametumia haki yake ya kuomba pigano la pili na Fury, aliyemzidi nguvu kupitia wingi wa pointi mjini Duesseldorf Novemba mwaka jana. Fury alisema ndoto zake tangu alipokuwa mtoto, zilikuwa ni kuwa bingwa wa heavyweight. "Vladimir sio bondia wa kujituma. Hapendi kujiingiza katika hatari yoyote hivyo huenda akazungumzia mchuano mzuri anaotaka kujaribu kupigana lakini sijawahi kumwona akifanya hivyo katika mapigano yake yote. Pigano pekee la kuburudisha alilowahi kuwa nalo ni wakati alishindwa kwa njia ya knock out. Hicho ndio kinachofanyika wakati akijaribu kupigana. Kwa hivyo namsubiri sana.

Fury atapanda ulingoni na dhidi ya Klitschko mjini Manchester mnamo Julai 9.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/DPA
Mhariri: Iddi Sessanga