Klitschko asema hayuko tayari kustaafu | Michezo | DW | 24.04.2017
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Michezo

Klitschko asema hayuko tayari kustaafu

Bingwa wa zamani wa masumbwi Wladmir Klitschko hana mipango yoyote ya kuteremsha pazia kwa taaluma yake ya miaka 21

Klitschko anasema anafurahia shinikizo linalomkabili kabla ya pigano lake la kuwania taji dhidi ya Muingereza Anthony Joshua.

Klitschko, ambaye hakuwahi kushindwa kwa miaka 11 kabla ya kuzabwa na Tyson Fury mwaka wa 2015, ameshinda mapigano 64 na kushindwa mara nne na atatatumai kulitwaa taji la Joshua la WBF uzani wa heavyweight pamoja na mataji yasiyomilikiwa na mtu kwa sasa ya WBA na IBO.

Mukraine huyo mwenye umri wa miaka 41 amesema anajiskia vizuri kiafya na motisha kubwa hivyo hana nia ya kustaafu kwa sasa. Klitschko atazirusha ngumi dhidi ya Joshua mnamo Aprili 29 mbele ya umati wa watu 90,000 uwanjani Wembley.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/DPA/Reuters
Mhariri: Iddi Ssessanga

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com