1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kiswahili Kina Wenyewe: Mpishano wa Kitikuu na Kisanifu

27 Novemba 2019

Kiswahili Sanifu si ulimi pekee wa lugha hii pana na tajiri ya wenyeji wa pwani ya Afrika Mashariki. Zipo ndimi nyengine nyingi, na mojawapo ni Kitikuu, lugha inayozungumzwa kwenye visiwa vya Lamu, upande wa kaskazini. Dk. Rukiya Saleh wa Chuo Kikuu cha Pwani nchini Kenya anafafanuwa namna Kitikuu kinavyojipambanuwa kwenye matumizi yake ya wakati na hali kutoka Kiswahili Kisanifu.

https://p.dw.com/p/3TnoL