KISMAYO:Kismayo bado kunatisha | Habari za Ulimwengu | DW | 04.10.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

KISMAYO:Kismayo bado kunatisha

Wanamgambo wa kiislamu nchini Somalia wamefanya maandamano makubwa katika mji wa Kismayo leo ambapo maelfu ya watu walihudhuria kupinga mipango ya kupelekwa kikosi cha kulinda amani.

Wanamgambo hao wamewaambia wafuasi wao wataanzisha vita vitakatifu dhidi ya kundi lolote litakalodhubutu kusimamisha maendeleo yake ya kijeshi.

Hii imekuja siku moja baada ya wanamgambo wanaiunga mkono serikali dhaifu ya Somalia kuapa kuukomboa mji huo wa bandari.

Wanamgambo hao waliuteka mji wa Kismayo wiki iliyopita bila ya kutokea umwagikaji wa damu.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com