Kipute cha Wimbledon chang′oa nanga | Michezo | DW | 01.07.2019
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Kipute cha Wimbledon chang'oa nanga

Kinyang'anyiro cha Wimbledon katika mchezo wa Tennis kiling'oa nanga Jumatatu huko Uingereza. Macho yote yatakuwa kwa Muingereza Andy Murray aliyerudi kutoka kwenye jeraha lililomuweka nje kwa miezi mitano.

Murray ambaye ni raia wa Scotland ana miaka 32 na anasema hatarajii mengi.

"Ningependa kufanya vyema nitakapokuwa uwanjani. Nacheza kwa ajili ya kupata ushindi na mimi ni mshindani sana. Lakini sijiambii kwamba, wiki nne au tano zilizopita nilikuwa sijui kama ningecheza hapa. Kwa hiyo sitarajii mengi. Lakini mara nitakapoingia uwanjani, nitajaribu kushinda kila mechi nitakayocheza," alisema Murray.

Wakati huo huo Mjapani Naomi Osaka ambaye alikuwa mchezaji nambari moja duniani upande wa kina dada anasema akili yake kwa sasa iko huru kutokana na shinikizo la kuitetea nafasi yake kama mchezaji nambari moja.

Tennis Australian Open Finale Frauen | Naomi Osaka

Osaka kwa sasa anaorodheshwa katika nafasi ya pili duniani

"Ndiyo, kisaikolojia kuwa nambari moja lilikuwa ni shinikizo kubwa sana kuliko nilivyotarajia. Kwa hiyo, ndio, nafikiri ni vyema kwangu kwa sasa kuorodheshwa wa pili hapa kwasababu jambo zuri ni kwamba ukishinda kipute hiki basi moja kwa moja unakuwa nambari moja. Kwa kweli hilo ndilo lengo langu kubwa. Sihitaji kufikiria kuhusu kuitetea nafasi yangu au kitu chochote," alisema Osaka.