Kiongozi wa zamani wa waasi Kongo afunguliwa mashtaka
12 Novemba 2025
Mashtaka hayo yanahusiana na ukatili uliofanywa mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo zaidi ya miongo miwili iliyopita.
Lumbala aliye na umri wa miaka 67 anatuhumiwa kushirikiana na wengine kufanya uhalifu dhidi ya binadamu wakati wa vita vya kati ya mwaka 1998 hadi 2003.
Makundi ya haki za binadamu yamesifu hatua ya kufunguliwa mashtaka kwa Lumbala wakidai ni fursa ya kuzuia unyanyasaji zaidi kufanyika huko mashariki mwa Kongo.
Mahakimu wanaochunguza kesi hiyo wanamuelezea Lumbala kama mbabe wa kivita aliyewakubalia wapiganaji wa kundi lake la waasi lililoungwa mkono na Uganda la RCD-N, kuuwa, kubaka na kufanya unyanyasaji wa aina nyengine kwa raia wa mashariki mwa Kongo.
Lumbala ambaye mwaka 2006 aligombea urais na kuhudumu kama waziri kabla kuachishwa kazi kutokana na ufisadi, anasisitiza kuwa alikuwa mwanasiasa wa kawaida tu ambaye hakuwa na wanajeshi chini yake.