Kimetto, Kipsang kushiriki London marathon | Michezo | DW | 09.01.2015
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Michezo

Kimetto, Kipsang kushiriki London marathon

Dennis Kimetto, aliyevunja rekodi ya ulimwengu ya marathon mwaka jana, na Mkenya mwenzake na bingwa mtetezi Wilson Kipsang, ambaye rekodi yake ilivunjwa na Kimetto, watashiriki mbio za London marathon

Kimetto ambaye alitumia muda wa saa mbili, dakika mbili na sekunde 57 katika mbio za mwezi Sepotemba mwaka jana za Berlin marathon na kuivunja rekodi ya Kipsang ya mwaka wa 2013 kwa kuondoa sekunde 26, atashiriki mbio za Marathon za London mnamo mwezi Aprili, kwa mara ya kwanza, wakati Kipsang akitafuta taji lake la tatu baada ya kushinda katika mwaka wa 2012 na 2014.

Wanariadha hao wawili wanafanya mazoezi ya pamoja katika mji wa Iten, nchini Kenya lakini hawajawahi kushindana katika mbio za marathon.

Muethiopia Kenenisa Bekele, bingwa wa Olimpiki na Ulimwengu wa mbio za mita 10,000 na 5,000 ambaye anashikilia rekodi ya ulimwengu, pia atashiriki kwa mara ya kwanza katika mbio za London Marathon. Mkenya Emmanuel Mutai ambaye alishinda mbio hizo za London mwaka wa 2011 pia atakuwa miongoni mwa washindani.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/reueters/AP
Mhariri: Iddi Ssessanga

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com