Kimbunga Aruba
2 Septemba 2007Matangazo
ARUBA
Kimbunga kilichopewa jina la ‚FELIX’ kilizidi kupata nguvu mapema asubuhi ya leo na kufikia kipimo cha daraja ya pili-kituo kinachochunguza vimbunga cha marekani kimearifu.
Hivyo kimekuwa kimbunga cha pili kuvuma msimu huu eneo hilo.Onyo la kimbunga limetolewa kwahivyo kwa kisiwa cha aruba,Bonaire na Curacao.