1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiMalawi

Kimbuga Freddy chauwa zaidi ya watu 100 Malawi, Msumbiji

14 Machi 2023

Kimbunga Freddy, kilichoambatana na upepo mkali na mvua kubwa, kimewaua zaidi ya watu 100 nchini Malawi na Msumbiji baada ya kuzipiga nchi hizo za kusini mwa Afrika.

https://p.dw.com/p/4Odqg
Malawi Mosambik Zyklon Tropensturm Freddy
Picha: Thoko Chikondi/AP Photo/picture alliance

Malawi ndio nchi iliyoathirika zaidi na kimbuga hicho, ambapo watu hadi sasa 99 wamepoteza maisha yao kufuatia maporomoko ya udongo yaliyosomba nyumba kadhaa nchini humo.

Kamishna katika idara ya kukabiliana na majanga Charles Kalemba amewaambia waandishi wa habari kuwa, wanatarajia idadi hiyo kuongezeka.

Kalemba ameeleza kuwa, watu 134 wamejeruhiwa na wengine 16 hawajulikani waliko. Tayari mji mkuu wa kibiashara wa Malawi Blantyre umerekodi vifo 85 viliyotokana na kimbunga hicho.

Shughuli za uokozi zingali zinaendelea huku wakaazi wakiripotiwa kutumia mikono yao kuchimba wakiwa na matarajio ya kupata manusura zaidi.