Kijana mmoja auawa katika kamatakamata Zanzibar | Matukio ya Afrika | DW | 29.10.2012
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Afrika

Kijana mmoja auawa katika kamatakamata Zanzibar

Visiwani Zanzibar operesheni ya kuwasaka wale wanaovuruga amani bado linaendelea.

Mji Mkongwe wa Zanzibar

Mji Mkongwe wa Zanzibar

Wakati jeshi la Polisi visiwani Zanzibar likiendelea kuwasaka wahalifu, baadhi ya wananchi wamejitokeza kulalamikia juu ya operesheni hiyo ikiwemo ukiukwaji wa haki za binadamu unaofanywa na jeshi hilo uliosababisha kifo cha kijana mmoja akiwa mikononi mwa polisi. Polisi nalo linakanusha kuhusika na mauaji hayo. Mwandishi wetu wa Zanzibar, Salma Said, amezungumza na wazee wa kijana huyo, Hamad Ali Kaimu, na kututumia taarifa kutoka huko. Na pia Sudi Mnette amezungumza na Kamanda wa Polisi wa Zanzibar, Mussa Ali Mussa, ambaye amekanusha kuhusika kwa jeshi lake. (Kusikiliza ripoti ya Salma Said na mahojiano ya Sudi Mnette, tafadhali bonyeza alama ya spika za masikioni hapo chini)

Mhariri: Mohamed Abdulrahman

Sauti na Vidio Kuhusu Mada