Kibaki ahidi serikali safi | Habari za Ulimwengu | DW | 12.12.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Kibaki ahidi serikali safi

NAIROBI.Akikabiliwa na kushuka kwa umaarufu, Rais Mwai Kibaki wa Kenya amesema kuwa atachagua viongozi wasafi katika serikali yake mpya iwapo atachaguliwa tena, ili kumsaidia katika vita dhidi ya rushwa.

Akihutubia katika siku ya uhuru wa nchi hiyo Rais Kibaki mwenye umri wa miaka 75 amesema kuwa atakuwa makini kurudisha imani ya serikali yake ambayo heshima yake imekuwa ikipungua kutokana na shutuma kuwa inakumbatia rushwa.

Rais Kibaki pia aligusia suala la amani wakati wa uchaguzi huo.

Kenya itafanya uchaguzi wake mkuu wa rais, wabunge na madiwani tarehe 27 mwezi ambapo Rais Kibaki anachuana vikali na Kiongozi wa chama cha upinzani cha ODM Raila Odinga.

Kura za maoni za hivi karibuni zinaonesha kuwa Raila Odinga anaongoza kwa asilimia chache dhidi Rais Kibaki huku waziri wa zamani wa mambo ya nje Kalonzo Musoka akiwa mbali.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com