Kenya:Rais Kenyatta atakiwa kuwepo ICC | Matukio ya Afrika | DW | 27.11.2013
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Afrika

Kenya:Rais Kenyatta atakiwa kuwepo ICC

Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu ICC imeubatilisha uamuzi ambao ulimkubalia Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta kuhudhuria baadhi tu ya vikao vya kesi yake, ikisema kuwa kiongozi huyo ni lazima afike mahakamani.

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta

Mahakama hiyo imetoa uamuzi kuwa kutokuwepo Kenyatta mahakamani kunaruhusiwa tu kutokana na mambo ya dharura na yenye umuhimu mkubwa. Mnamo Oktoba 18 majaji walimruhusu Kenyatta kutohudhuria vikao kwa sababu ya shambulizi la kigaidi katika jumba la maduka la Westgate, na wiki mbili baadaye, mahakama hiyo ikaahirisha tarehe ya kuanza vikao vyake baada ya mawakili wa Kenyatta kusema shambulizi la Westgate lilizusha mgogoro wa kitaifa na kimataifa. Bruce Amani amezungumza na wakili wa mahakama Kuu nchini Kenya, Agina Ojwang, na kwanza alitaka kusikia maoni yake kuhusiana na uamuzi huo wa ICC. Kusikiliza mazungumzo hayo bonyeza alama ya spika za masikioni hapo chini.

Mwandishi: Bruce Amani

Mhariri: Josephat Charo

Sauti na Vidio Kuhusu Mada