Kenya: Uchunguzi wa kifo cha Mutula Kilonzo wafanyika leo
29 Aprili 2013Kulingana na Mtaalamu wa uchunguzi wa sababu za kifo Johansen Oduor amesema uchunguzi huo kwa sasa utajikita zaidi katika chakula cha mwisho alichokula Marehemu Kilonzo..
Mutula Kilonzo ambaye alikuwa waziri katika serikali iliopita, alikutwa chumbaniJumamosi asubuhi akiwa amefariki huku mapofu yakimtoka mdomoni na puani. Msemaji wa familia yake Chris Musau amesema mipango ya mazishi itafanyika wakati ukapomalizika.
Jee wa kenya watamkumbuka vipi marehemu Mutula Kilonzo? Amina Abubakar amezungumza na Professa Tom Namwamba ambaye ni mchambuzi wa maswala ya kisiasa akiwa Nairobi na kwanza ana haya ya kueleza. Kusikiliza mazungumzo hayo bonyeza alama ya spika za masikioni hapo chini.
Mwandishi: Amina Abubakar
Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman