Kenya: Tishio la mashambulizi ya kigaidi mjini Mombasa
16 Mei 2014Matangazo
Hatua hii imechukuliwa baada ya ofisi ya mambo ya kigeni ya Uingereza kusema raia wake lazima waondoke kutokana na vitisho vya mashambulizi ya kigaidi. Tayari watalii hao wameanza kuondoka mjini humo huku baadhi ya washikadau wa sekta ya utalii wakisema hatua hio huenda ikayumbisha sekta hiyo nchini Kenya. Kupata zaidi juu ya hayo Amna Abubakar amezungumza na meneja wa hoteli moja mjini Mombasa Daudi Nyamu na kwanza anaelezea juu ya athari za hatua hiyo iliochukuliwa na shirika la usafiri la Uingereza. Kusikiliza mazungumzo hayo bonyeza alama ya spika za masikioni hapo chini.
Mwandishi: Amina Abubakar
Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman