1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kenya: Mwanasiasa auwawa Kisumu

30 Oktoba 2012

Kenya imeripotiwa kwamba watu watatu wameuwawa na wengine kadhaa wamejeruhiwa kufuatia maandamano yaliyogeuka kuwa vurugu hapo jana (29.10.2012) baada ya kuuwawa kwa mgombea wa ubunge wa chama cha ODM,Shem Onyango Kwega.

https://p.dw.com/p/16ZLS
Ghasia mjini Kisumu baada ya kuuwawa Shem Onyango
Ghasia mjini Kisumu baada ya kuuwawa Shem OnyangoPicha: AP

Mwanasiasa huyo maarufu katika eneo hilo la Kisumu Magharibi alipigwa risasi na watu wasiojulikana alipokuwa katika gari lake pamoja na mkewe ambaye kwa sasa anapata matibabu katika hospitali moja mjini humo.Kujua zaidi hali ilivyo mjini Kisumu Amina Abubakar amezungumza na mwandishi habari mmoja katika eneo hilo Maureen Akinyi.

(Kusikiliza mazungumzo bonyeza alama ya spika za masikioni hapo chini)

Mwandishi: Amina Abubakar

Mhariri: Yusuf Saumu