Karandinga: Wawindaji Haramu | IDHAA YA KISWAHILI | DW | 15.02.2017
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

IDHAA YA KISWAHILI

Karandinga: Wawindaji Haramu

Afisa upelelezi Allan anachunguza kuchomwa kisu kwa daktari wa wanyama Patrick. Mwenzake Carl anamsaka Bwana G – mkuu wa mtandao wa ujangili unaosababisha athari kubwa huko Bovu.

Wanawaua kinyama: tembo, chui na faru na aina nyingi za wanyama hawa ziko hatarini kutoweka kabisa. Mfumo wa viumbe hai unaathirika pamoja na uchumi huku majangili wakijipatia mamilioni ya fedha. Allan anafuata njia nyingi lakini Carl anakabiliwa na changamoto kubwa kwa sababu hakuna anayefahamu utambulisho halisi wa Bwana G. Kwa mshangao wa maafisa hao wawili wa upelelezi, kesi inakamilika wakati barua ya usaliti inapogunduliwa katika vitu vya Patrick inayotishia kufichua utambulisho halisi wa Bwana G. Je muhanga wa mauaji alijua Bwana G ni nani hasa? Je huenda hii ndiyo sababu kwa nini alitakiwa kufa? Hatimaye ukweli unajitokeza kuwa wa kushangaza zaidi. Je kipi kitakachotokea? Fuatilia mchezo huu kuanzia mwanzo hadi mwisho wake.

 

 

Sauti na Vidio Kuhusu Mada

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com