Karandinga: Siri ya Mifupa | Noa Bongo | DW | 20.03.2018
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Noa Bongo

Karandinga: Siri ya Mifupa

Zuri, mtoto mwenye umri wa mwaka mmoja anatekwa usiku wa manane nyumbani kwa wazazi wake.

Wakati Zuri anatekwa usiku wa manane kwenye mtaa wa mabanda, wazazi wake wanahuzunika. Nani atakuwa amemtaka mtoto wao wa kiume na kwa nini? Watoto kadhaa katika eneo hilo ambao awali walipotea katika mazingira ya kutatanisha, hawakupatikana tena. Polisi wanaanza haraka kumtafuta Zuri. Aina fulani ya ushahidi unamnyooshea kidole Lindia, mganga wa kienyeji, lakini anadai kwamba hana hatia. Baba yake Zuri anamuomba mganga mwingine wa kienyeji, Shava, amsaidie kumtafuta mtoto wake. Shava anajulikana katika jamii hiyo na inasemekana ana nguvu sana. Mganga yupi kati ya hao wawili ni mkweli na anaweza kuaminiwa? Na je, juhudi za kumpata Zuri akiwa hai zitafanikiwa?

Sauti na Vidio Kuhusu Mada

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com