Karandinga: Kuisafisha Likalongo | Karandinga | DW | 21.02.2019
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Karandinga

Karandinga: Kuisafisha Likalongo

Watu wanatupa takataka hovyo kwenye jaa pekee la taka la Zukosso kwenye wilaya ya huko Sanosso. Kutokana na kujaa kupita kiasi, maporomoko yanatokea na kusababisha maafa makubwa ikiwemo vifo.

Kwa mshangao wake, mjasiriamali kijana wa Kiafrika Randolph anakamatwa kufuatia maporomoko yaliyotokea kwenye kituo cha kutupa taka katika mji ambacho hakijadhibitiwa.

Anatwikwa lawama za waathirika 27 wa maporomoko hayo– wakati alichokitaka ni kupunguza na kurejelea taka kupitia kampuni yake ya huduma za ukusanyaji taka ya Sanosso Eco Agency. Rosa, mwanablogi wa kimazingira, pamoja na marafiki zake Randolph, Mathilda na Rama, wanajaribu kuthibitisha kuwa Randolph hana hatia.

Wakati wa harakati zao zilizokumbwa na matatizo, wanagundua kuwa suala hilo ni zaidi ya usimamizi wa taka. Wanawabaini pia watu waliotaka kumtumia Randolph ili kuficha makosa yao. Mchezo huu umeandikwa na Hurcyle Gnonhoué kutoka Bénin.

Sauti na Vidio Kuhusu Mada