Karandinga: Inaihusisha Jamii | Karandinga | DW | 04.03.2020
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Karandinga

Karandinga: Inaihusisha Jamii

Mchezo huu unahusu haki za watoto. Fahamu zaidi kuhusu ndugu wawili wa kike, Jane na Hope pamoja na mama yao, Carol. Wanaishi katika wakati mgumu sana. Kwa nini? Na watafanya nini? Ungana nasi....

Wasichana ndugu Hope na Jane wanaonekana kuishi maisha ya kawaida katika mji mdogo wa Kiafrika pamoja na mama yao. Mama yao anapofariki, wasichana hao wanaishi peke yao bila kumuambia yeyote. Wakati wakijaribu kuonesha kuwa kila kitu kiko sawa, Jane na Hope wanaingia katika matatizo zaidi. Marafiki zao, watoto wa mitaani Sara na Leroy wanajaribu kuwasaidia, lakini hatimaye siri yao inafichuka. Baba wa wasichana hao anajitokeza. Alikuwa akiinyanyasa familia yake, na ndiyo sababu walikimbia. Je, ndugu hao watapata msaada wanaouhitaji kulinda haki zao? Mchezo huu umeandikwa na Carla Fernandes kutoka Angola.

Sauti na Vidio Kuhusu Mada