Karandinga: Chozi la Mnyonge | Karandinga | DW | 01.03.2017
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Karandinga

Karandinga: Chozi la Mnyonge

Katika mji wa Lambu, ghafla polisi wana mambo mengi ya kufanya: Mtoto mchanga amekutwa tu nje ya kituo cha polisi.

Siku inayofuata, mtu anayeheshimika sana katika jamii anakutwa amekufa mbele ya nyumba yake, huku kisu kikiwa bado kwenye kifua chake. Afisa kijana wa polisi, Amsa, anazishughulikia kesi hizo akishirikiana na mpelelezi mkuu, Bruce. Akiwa polisi pekee wa kike wa Lambu, Amsa pia anafuatwa na wanawake kadhaa wanaonyanyaswa na anajitolea kuwasaidia. Hili ni jambo gumu kwa sababu bado hakuna sheria kwenye nchi hiyo inayowaadhibu watu wanaofanya unyanyasaji wa majumbani. Ungana na Amsa, akijaribu kushughulikia kesi hizo na kuwalinda waathirika wa unyanyasaji wa majumbani.

 

Sauti na Vidio Kuhusu Mada

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com