Karandinga: Biashara Chafu | Karandinga | DW | 21.02.2019
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Karandinga

Karandinga: Biashara Chafu

Mchezo huu unahusu athari za ufisadi, ambapo Zita, binti mwenye umri wa miaka 22. Zita anasomea sheria katika Chuo Kikuu cha Bazingo. Na hapa anataka kuitumia taaluma yake kupambana na mafisadi. Wacha tujiunge na Zita.

Zita na familia yake wanapoteza kila kitu katika moto ulioteketeza eneo wanakoishi la makaazi ya watu wenye kipato cha chini. Baadhi ya majirani wanadhani ilikuwa ajali, lakini Zita, mwanafunzi kijana anayesomea sheria, anaanzisha uchunguzi kubaini mhusika.

Anagundua kuwa siyo tu makaazi yake ya zamani, bali hata sehemu kubwa ya miundombinu ya mji huo ilijengwa kupitia mikataba ya rushwa, kwa kupuuza viwango vya usalama na kuwaweka raia katika hatari.

Anaanzisha kampeni kupitia mitandao ya kijamii kufichua uozo huo na kuongeza uhamasishaji – hatua inayomaanisha kujiweka katika hatari, na muda si mrefu anaanza kupokea vitisho.

Je, msichana huyo alimega zaidi ya anachoweza kutafuna au kweli ataweza kuleta tofauti katika mapambano dhidi ya rushwa? Mchezo huu umeandikwa na Chrispin Mwakideu kutoka Kenya.

Sauti na Vidio Kuhusu Mada