1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kansela Scholz kukutana na Netanyahu nchini Israel

17 Machi 2024

Maandalizi ya Israel kufanya operesheni ya pili ya ardhini katika mji wa Rafah kusini mwa Ukanda wa Gaza yatajadiliwa. Scholz anatarajiwa kutoa tahadhari ya dharura kuipinga opereshdni hiyo.

https://p.dw.com/p/4dofm
Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz anaitembelea Jordan na Israel
Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz anaitembelea Jordan na IsraelPicha: Kay Nietfeld/dpa/picture alliance

Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz anatazamiwa hii leo kukutana na Mfalme Abdullah II wa Jordan katika ziara yake katika nchi hiyo ya Mashariki ya Kati. Baadaye jioni, atasafiri kuelekea Tel-Aliv ambako atakutana na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu na Rais Isaac Herzog.

Scholz anatarajia kuzungumza na viongozi hao kuhusu mipango ya kuwasilishwa kwa misaada ya kibinadamu katika Ukanda wa Gaza pamoja na suala la makubaliano ya usitishaji mapigano. Pia, atakutana na familia za baadhi ya mateka ambao bado wanashikiliwa na kundi la Hamas huko Gaza.

Soma pia: Israel yaidhinisha operesheni ya kijeshi Rafah

Maelfu ya watu waliandamana jana usiku mjini Tel Aviv na katika miji mingine ya Israel wakitaka kufikiwe makubaliano yatakayowezesha kuachiliwa huru kwa mateka zaidi. Mazungumzo yaliyokwama ya kusitisha vita kati ya Israel na Hamas yanatarajiwa kuanza tena hii leo nchini Qatar.