Kandoni mwa G-8 Heligendemam | Masuala ya Jamii | DW | 07.06.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Masuala ya Jamii

Kandoni mwa G-8 Heligendemam

Polisi ya watia nguvuni wakereketwa 300 kwenye mkutano wa kilele wa kundi la G-8 huko Heiligendamm,Ujerumani.Vijana nao wamekutana na viongozi na kutoa mapendekezo yao.

Kanzela Merkel na rais Putin katika G-8

Kanzela Merkel na rais Putin katika G-8

Katika siku ya pili ya mkutano huo wa kundi la mataifa 8-tajiri huko Heiligendamm,mashariki mwa Ujerumani,polisi leo imewatia nguvuni waandamanaji 300 na ikatumia tena mabomba ya maji kuwalazimisha kujitenga na barabara zinazoelekea kituo cha mkutano cha heiligendamm,kandoni mwa pwani ya bahari ya Baltik.

Pia ujumbe wa vijana kutoka nchi mbali mbali ulipata nao fursa adhuhuri ya leo kuonana na viongozi wa dola hizo 8 na kusikiliza mapendekezo yao.

Vijana hao walijipatia nafasi hiyo kutokana na mashindano yalioendeshwa na shirika la UM linalohudumia watoto-UNICEF na mnamo siku chache zilizopita wakizungumzoa mada za kikao hiki cha G-8 kama vile kupiga vita umasikini,uchafuzi wa hali ya hewa na maradhi ya UKIMWI.Jukwaa lao lakini lilikuwa ndani ya marekebu maalumu ilioegesha bandarini mjini Wismar.

Ujumbe wa vijana wa Ujerumani uliingiza msichana wa miaka 16 Lisa Marie Ullrich alielezea hivi wasi wasi wa vijana na mahitaji yao:

“Mnamo siku chache zilizopita tukiwa kama vijana, tulikaa pamoja na kuzingatia mada hizo.Na sasa, tunafurahi kuwaarifu mapendekezo yetu.Tunawaomba muzingatie mashauri yetu na labda, mojawapo ya mashauri hayo muyaingize katika maazimio yenu mtakayopitisha ili nasi vijana tuwe tumechangia katika kunoa mustakbala wetu.”

Ellen McCoy kutoka Uingereza alivizindua viwanda juu ya jukumu lao la kiadilifu aliposema:

“Kila kiwanda kinabeba dhamana kwa bidhaa zake kinachotengeza kwa mazingira,mahala kilipo na kwa wafanyikazi wake.”

Pamoja na vijana wengine, Ellen McCoy alishauri viwanda na makampuni yanayotengeza bidhaa zao kwa kutia maanani hali za jamii na mazingira zipewe nafuu za kodi.

Kanzela Angela Merkel aliowalahki vijana hao aliojibu:

“Tumeahidiana leo kuwa, daraja zote zilizowekwa na ILO-yaani shirika la kazi ulimwenguni ambazo zimegeuka pia ni za Umoja wa Mataifa, tuziheshimu ili uwepo utandawazi wa haki ulimwenguni.”

Risala kutoka mkutano wa UKIMWI mjini Durban,Afrika Kusini kwa viongozi wa dunia wa kundi la G-8 inawataka kukodolea macho juhudi za kupiga vita Ukimwi mbali ya kwamba jukumu lake kubwa ni kuzingatia huko Heiligendamm mada nyengine za maendeleo.

Mkurugenzi wa shirika la afya ulimwenguni (WHO) wa maradhi ya UKIMWI, Kevin de Cock amesema kuna hatari za machofu kuzungumzia maradhi ya Ukimwi na hivyo kukaiweka mada hiyo pembeni kabisa.

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com