Kampeni za uchaguzi mkuu zapamba moto | Magazetini | DW | 14.09.2009
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Magazetini

Kampeni za uchaguzi mkuu zapamba moto

Mdahalo wa televisheni ulikua chapwa kati ya Angela Merkel na Frank-Walter Steinmeier

default

Kansela Angela Merkel na mpinzani wake Frank-Walter Steinmeier

Wiki mbili kabla ya uchaguzi mkuu,wagombea wawili wakuu wa kiti cha kansela,bibi Angela Merkel wa kutoka chama cha CDU na Frank-Walter Steinmeier wa kutoka chama cha SPD walishindana jana usiku kwa njia ya televisheni kubainisha nani ana hoja kali kumshinda mwenzake katika wakati huu wa shida za kiuchumi.Wahariri wa magazeti ya Ujerumani walikua na kazi ngumu ya kumchagua mshindi wa mdahalo huo.Magazeti mengi pia yamesikitishwa na ile hali kwamba mdahalo huo haukua wa kusisimua na kuna wahariri wanaofika hadi ya kubisha kama kweli ulikua mdahalo na sio mazungumzo.

Tuanze basi na gazeti la "SÜDDEUTSCHE ZEITUNG" lililohisi kama kulikua na mdahalo basi kati ya wanasiasa na waandishi habari.Waandishi habari wote wanne hawakufuata mtindo wa kimarekani kuwaachia washirika wazungumze mpaka mwisho.Hata hivyo SÜDDEUTSCHE ZEITUNG linasema kuna aliyeibuka na ushindi:

"Frank Walter Steinemeier amefanya vizuri zaidi kuliko vile ilivyokua ikitarajiwa.Alikua akitoa hoja kali kali bila ya malumbano.Ameonekana uongozi wa taifa anauweza,na alikua mcheshi na mwenye haiba." Kinyume na kansela ambae kwa mshangao wa wengi ameonekana kama anajitetea, hana raha..."

"Spiegel Online lina maoni sawa na hayo.Linahisi zilikua "dakika 90 za kujisifu".Hakujakua na mdahalo hata kidogo, limeandika gazeti la Spiegel kaatika mtandao wake.

Angela Merkel hakutumia fursa aliyokua nayo kama mtetezi wa kiti cha kansela.Zaidi ya hayo kuna masuala ambayo hajayajibu-kwa mfano kwanini vyama ndugu vya CDU/CSU vinakihitaji "kwa kila hali "chama cha FDP kama mshirika mpya serikalini".

Gazeti hilo la mtandao linaungama Steinemeier ameitumia vyema fursa aliyoipata hasa katika mada inayohusu uchumi na jamii.Gazeti linaendelea kuandika:

Angalao amefafanua kwanini chama cha SPD kinahitajika serikalini.Kwasababu kinatetea masilahi ya jamii.Amechambua vilivyo na kwa namna ya kuaminika hoja za Merkel,ambazo kawaida hutolewa na chama cha FDP zinazoshadidia juu ya"fedha taslim kwa wingi kwasababu ya kiwango kikubwa cha fedha bila ya kodi."Hapo Steinmeier alitia fora kweli kweli kwa hoja zake.

Hata gazeti la mjini FRANKFURT linamtaja Steinemeier kua mshindi wa mdahalo huo wa jana usiku.Gazeti linaendelea kuandika:

Steinmeier amefanya vyema zaidi-amefanya vuziri kuliko watu walivyokua wakitarajia.Lakini pengine wasimamizi wa mdahalo huo ndio wa kukosolewa kwasababu walionyesha kumpendelea zaidi,hata masuala waliyokua wakimuuliza yalikua afadhali na hawakua wakimkata sana alipokua akijibu.

Angela Merkel Frank-Walter Steinmeier TV Duell Fernsehduell Flash-Galerie

Kiti moto katika televisheni

Nalo gazeti la mjini Cologne -Kölner Stadt Anzeiger linaandika

Walikua wababe waliokua wakipigana bila ya mapanga.Mtu anaweza kusema walikua kama mke na mume ambao baadhi ya wakati wanagombana lakini kwa jumla wanasikilizana vizuri.

Mwandishi:Hennen,Claudia (ZRP) O.Hamidou

Mhariri:M.Abdul-Rahman