KAMPALA:Watu 4 wauawa 6 kujeruhiwa kwenye mlipuko jaani | Habari za Ulimwengu | DW | 24.07.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

KAMPALA:Watu 4 wauawa 6 kujeruhiwa kwenye mlipuko jaani

Raia wanne wa Uganda wamepoteza maisha yao na wengine 6 kujeruhiwa baada ya kifaa kimoja kulipuka kwenye jaa la vyuma vya zamani. Kwa mujibu wa msemaji wa jeshi Meja Felix Kulaigye kifaa hicho kililipuka wakati taka hizo zilikuwa zinahamishwa kwenye kambi moja kaskazini mwa Uganda.

Vita kati ya serikali na waasi wa Lords Resistance Army LRA nchini humo vilivyodumu kwa miaka 20 viliacha mabomu ya kutegwa ardhini na vifaa vingine vya kulipuka katika eneo la kaskazini mwa Uganda.

Mabomu hayo hayajatumika kwenye shughuli za kijeshi kwa muda mrefu ila bado yanasababisha matatizo kwa wakazi wa eneo hilo waliorudi baada ya vita kumalizika.Mazungumzo ya amani kati ya serikali na Waasi hao wa LRA yalianza miaka miwili iliyopita.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com