KAMPALA Wahindi mashakani | Habari za Ulimwengu | DW | 13.04.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

KAMPALA Wahindi mashakani

Wahindi wa jamii ya Uganda hawakupeleka watoto shule, kufunguwa maduka yao au kurepoti kazi leo hii kwa kuhofia kurudiwa kwa matukio ya jana ambapo kundi la watu limewapiga mawe hadi kufa wahindi wawili.

Maadamano ya kupinga kuuzwa kwa Msitu wa Mabira katika mji mkuu wa Kampala hapo jana yaligeuka kuwa ghasia za kibaguzi na kuwalazimisha polisi kufyetuwa mabomu ya kutowa machozi pamoja na kuuwa kwa kuwapiga risai watu wawili.

Wahindi waliouwawa hawana uhusiano na kampuni ya Mehta Group inayoendeshwa na Mganda wa asili ya kihindi ambayo inataka kutumia hifadhi ya misitu ya Mabira kwa ajili ya kutanuwa shughuli zake za kuzalisha miwa.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com