Kabul.Uingereza yaondosha vikosi vyake huko mkoa wenye machafuko nchini Afghanista. | Habari za Ulimwengu | DW | 17.10.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Kabul.Uingereza yaondosha vikosi vyake huko mkoa wenye machafuko nchini Afghanista.

Vikosi vya kijeshi vya Uingereza vimeondoshwa kutoka katika mkoa wenye machafuko kusini mwa Afghanistan, kufuatia ombi lililotolewa na wakuu wa kikabila katika eneo hilo.

Musa Qala aliyepo katika mkoa wa Helmand, amesema kuwa, mkoa huo ni sehemu mbaya zaidi katika nchi hiyo na kumeshuhudiwa mapigano makali kati ya vikosi vya NATO na wanamgambo wa Kitaliban.

Msemaji wa NATO amesema kuondoka kwao mkoani humo kunatokana na maombi ya Gavana wa mkoa huo.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com