Josephat Charo | Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili | DW | 20.04.2017
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Timu ya DW Kiswahili

Josephat Charo

Mfahamu Josephat Charo, mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW.

 1. Nchi ninayotokea: Kenya
 2. Mwaka nilipojiunga na DW: 2004
 3. Nilivyojiunga na DW: Nilijiunga na DW kwa mafunzo ya miezi sita Juni hadi Novemba 2004. Kuanzia Desemba mosi nikaanza kufanya kazi baada ya kupata mkataba.
 4. Kwanini niliamua kuwa mwandishi wa habari: Nipate mshahara kujikimu kimaisha. Ili nisafiri sana na niwe na fursa ya kukutana na kuzungumza na viongozi mashuhuri, watu wenye ushawishi katika jamii, watu wa matabaka yote na kuwapa sauti wale wasio na mtu wa kuwatetea. Nilitaka pia kuelimisha jamii na kuwafahamisha watu kuhusu matukio yanayoendelea ulimwenguni - yaliyo karibu na hata yale yaliyo mbali nao.
 5. Vigezo mtu anavyotakiwa kuwa navyo kuwa mwandishi wa habari: Elimu, kipaji na kipaji.
 6. Changamoto ninazokutana nazo kwenye maisha yangu ya kazi: Kutafuta mahojiano kwa njia ya simu na watu wenye dhamana wa jambo fulani ambao huna miadi nao. Tafsiri ya maneno mapya yanayojitokeza kila uchao hususan katika sekta ya teknolojia. Baridi kali na theluji kibao.
 7. Tukio la kihistoria ambalo sitalisahau: Kuchaguliwa kwa Barack Obama kuwa rais wa kwanza wa asili ya kiafrika wa Marekani.
 8. Mtu ambaye ningependa kumhoji: Michelle Obama
Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com