1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jeshi la DRC lachukua udhibiti wa vijiji vya wilaya ya Fizi

Mitima Delachance16 Agosti 2021

Jeshi la Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo limefanikiwa kudhibiti vijiji kadhaa vya wilaya ya Fizi vilivyokuwa chini ya waasi wa Twirwaneho na Gumino wanaodai kupigania maslahi ya kabila la Banyamulenge katika mkoa wa Kivu Kusini. Hata hivyo kabila la Banyamulenge, limelalamika kwamba watu wapatao 100 wa jamii hiyo ambao hawana hatia wameuawa katika makabiliano hayo ya Alhamisi iliyopita.

https://p.dw.com/p/3z2av