Janet Jackson ajifungua akiwa na miaka 50 | Masuala ya Jamii | DW | 04.01.2017
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Masuala ya Jamii

Janet Jackson ajifungua akiwa na miaka 50

Mwimbaji wa muziki wa "pop" nchini Marekani, Janet Jackson, amejifunguwa mtoto wake wa kwanza akiwa na umri wa miaka 50, kwenye ndoa yake ya tatu na bilionea wa Qatar, Wassim al-Mana.

"Janet na mumewe Wissam al-Mana wana furaha kubwa kumkaribisha mvulana mpya, Eissa al-Mana, hapa duniani." Inasema taarifa ya msemaji wa mwanamuziki huyo.

Janet aliiahirisha ziara yake ya tamasha la muziki la kimataifa kwa jina "Unbreakable" mwezi Aprili 2015, akiwaambia mashabiki wake kuwa yeye na mumewe walikuwa wanapanga mipango ya familia yao.

Mbali ya kuwa dada wa nyota muziki wa "pop" Marehemu Michael Jackson, Janet amekuwa pia na mafanikio yake mwenyewe, akiwa ametoa albamu saba zilizofikia kilele cha kushika nafasi ya kwanza na vile vile kupokea tuzo tano za Grammy.

Miongoni mwa nyimbo zake zilizoshika nafasi ya kwanza ni "All for You", "Again" na "Doesn't Really Matter."

Aliolewa na bilionea wa Qatar, Wissal al-Mana, mwaka 2012 ikiwa ni ndoa yake ya tatu. Anapanga kurudi kwenye ziara yake baada ya mapumziko ya uzazi, lakini hapajatolewa tarehe rasmi hadi sasa.

Mwandishi: Mohammed Khelef/dpa
Mhariri: Grace Kabogo

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com