Pressefreiheit Kriegsgebiete
26 Mei 2008
Waandishi wa habari ambao wanaandika habari zao katika maeneo ya vita na ya hatari huuwawa kila mara. Kwa hakika wanalindwa na sheria, lakini kivitendo , sio hivyo kama inavyoeleza taasisi isiyo ya kiserikali ya waandishi wasio na mipaka tawi la Ujerumani. Asasi inayotetea uhuru wa kutoa maoni duniani , imewaalika waandishi pamoja na wanaharakati wa kupigania haki za binadamu mjini Berlin , kulijadili suala kuhusiana na njia ya kupata utatuzi na sababu zinazoleta hali ya kuongezeka kwa hatari dhidi ya waandishi katika maeneo ya mizozo.
Wakati waandishi wa habari wanapotoa taarifa zao kutoka katika maeneo ya mizozo, taarifa hizo zinaonyesha hali halisi ya maeneo hayo. Kwa kufanya hiyo waandishi wanapojaribu kwa kadiri ya uwezo wao kueleza kwa undani, kufanya tathmini ya kina na ikiwezekana kuonyesha ukweli halisi, hawahitaji tu kuheshimiwa na kuthaminiwa. Ni lazima pia kupata ulinzi kutoka katika mataifa hayo yenye mizozo, anaelezea Günter Nooke, mjumbe wa serikali ya Ujerumani akihusika na masuala ya siasa za haki za binadamu na misaada ya kiutu katika wizara ya mambo ya kigeni.
Sio tu kwamba mataifa yanawajibu wa kulinda uhuru wa kutoa maoni, na haki za binadamu katika maeneo ya mizozo. Baada ya mizozo na kupata amani, na katika maeneo ambayo hayako katika lengo la juu la kisiasa, ni lazima serikali zionyeshe umuhimu wa juu katika utoaji habari huru na wa haki kuhusiana na vita na mizozo. Aina hii ya utoaji habari inaleta utatuzi wa haraka wa mizozo kutokana na kujua chanzo cha mizozo.
Mataifa pamoja na serikali mbali mbali zinazidi kuwaona waandishi wa habari ambao wanapaswa kuonekana kuwa wanachukua mtazamo wa kati katika maeneo yenye migogoro, kuwa wanawaharibia. Sio tu utaratibu wa kile kinachojulikana kama waandishi wanaoambatana na wanajeshi, lakini pia waandishi, ambao wanajiambatisha na kundi mojawapo katika mzozo fulani, wanajikuta katika hali isiyokuwa salama , kwa mfano maripota katika eneo la vita nchini Iraq.
Hali iko hivi siku hizi, wakati kunatolewa taarifa rasmi na inatangazwa moja kwa moja, inawezekana ikazimwa, na taarifa hiyo ikafanywa na kundi pinzani kuwa ni ya kutatanisha. Hii ina maana kuwa wakati tunaangalia vita vya ghuba , ama kile ambacho waandishi wamekuwa wakituletea hapo zamani, ni sehemu tu ya uongozi wa kivita wa Marekani, bila ya kile ambacho tumekuwa tukikipata hapo kabla.
Anasema Ulrich Tilgner , mmoja wa maripota wanaofahamika sana nchini Ujerumani na katika televisheni yenye sifa ya kutoa taarifa za uwazi. Wakati akifanyakazi katika eneo la mashariki ya kati, ameripoti kuwa , hata katika shirika la habari la Ujerumani kuna hali ya udhibiti. Pamoja na hayo si waandishi wachache ambao walilazimika moja kwa moja kuchunguzwa na mashirika mbali mbali ya ujasusi. Anawaona waandishi wa habari katika hali inayoongezeka ya hatari.
►◄