J3 0809 News | Habari za Ulimwengu | DW | 08.09.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

J3 0809 News

Washington . Bin Laden awataka Wamarekani kuukubali Uislamu.

Kiongozi wa kundi la kimataifa la kigaidi la al-Qaeda Osama bin Laden amewataka Wamarekani kuukubali Uislamu katika juhudi za kumaliza vita nchini Iraq.

Osama bin Laden alikuwa akizungumza katika video yake ya kwanza ambayo ameweza kuitangaza kwa muda wa miaka mitatu.

Mashirika ya ujasusi ya Marekani yamesema kuwa sauti katika ukanda huo inaonekana kuwa ni ya bin Laden.

Video hiyo imetolewa katika tovuti ya makundi ya harakati za Kiislamu siku chache kabla ya maadhimisho ya mwaka wa sita tangu kufanyika shambulio la Septemba 11 mwaka 2001 , mjini New York na Washigton. Wakati huo huo mkurugenzi wa shirika la ujasusi la CIA Michael Hayden ameonya katika hotuba kuwa shirika hilo linaamini kuwa al-Qaeda inapanga shambulio jipya na kubwa katika maeneo ya Marekani.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com