J2 0809 News | Habari za Ulimwengu | DW | 08.09.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

J2 0809 News

Warsaw. Wabunge wapiga kura kulivunja bunge.

Bunge la Poland limepiga kura kulivunja , na kusafisha njia kuelekea uchaguzi mwingine utakaofanyika miaka miwili kabla ya muda wake.

Wabunge wamepiga kura kwa zaidi ya wingi wa theluthi mbili unaohitajika kuunga mkono hoja hiyo.

Chini ya katiba ya Poland , rais Lech Kaczynski anatakiwa kupanga tarehe kwa ajili ya uchaguzi huo, ambao unatakiwa kufanyika sio zaidi ya Oktoba 21. Waziri wake mkuu ambaye ni pacha wake Jaroslav Kaczynski , amesema baadaye kuwa uchaguzi utatoa kwa wapigakura nafasi mpya ya kukipa madaraka chama chake kupambana na ulaji rushwa.

Maoni ya hivi karibuni ya wapiga kura yanaonyesha kuwa kampeni inaweza kutoa mpambano wa karibu kati ya chama tawala cha rais Kaczynski cha kihafidhina cha Sheria na haki na kile cha Civic Platform.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com