Ivory Coast | Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili | DW | 27.11.2010
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Timu Yetu

Ivory Coast

Uchaguzi nchini Ivory Coast.

default

Aliyekuwa waziri mkuu wa Ivory Coast, Alassane Ouattara katika kampeni za uchaguzi.

Wapinzani wakisiasa nchini Ivory Coast hapo jana walikamilisha mikutano ya kampeni za uchaguzi unaotarajiwa kufanyika hapo kesho na ambao unatarajiwa kumaliza mwongo mmoja wa kutoimarika kwa nchi hiyo inayogubikwa na hofu na umwagikaji damu.

Maelfu ya wafuasi walimiminika katika mikutano tofauti ya rais Laurent Gbabo na mpinzani wake Alassane Outtara katika mji mkuu wa  kibiashara wa Abidjan, ambao ni eneo kuu la upigaji kura katika nchi hiyo iliyogawanyika.

Präsidentschaftswahlen Elfenbeinküste Laurent Gbagbo

Rais Laurent Gbagbo, akiwasili katika kampeni.

Wagombea wa uchaguzi huo wametoa wito wa kupigwa kura kwa amani, lakini dalili za vurugu  zilionekana wakati kambi ya Outtara ilipokataa wito wa Gbabo wa kuwepo amri ya kutotembea baada ya uchaguzi wa kesho. Vikosi vya jeshi nchini humo na vya Umoja wa Mataifa  vimemiminika kuimarisha usalama iwapo patazuka vurugu.

Mwandishi :Maryam Abdalla/Afpe

Mhariri:Sekione Kitojo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com