1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ISTANBUL:Maelfu waandamana kutaka serikali isiyoegemea dini

6 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC4Z

Takriban watu elfu 90 wameandamana huko magharibi mwa Uturuki katika kuunga mkono taifa lisiloegemea upande dini.

Maandamano hayo katika miji ya Mabisa na Canakkale, yamefanyika siku moja kabla ya bunge kupiga kura kwa mara pili kumchagua rais, ambapo mgombea pekee ni waziri wa mambo ya nje Abdullah Gul muhafina wa zamani wa kiislam kutoka chama tawala cha AKP:

Waziri Mkuu wa Uturuki Tayyip Erdogan amependekeza mabadiliko ya katiba, yatakayowapa nafasi wananchi kumchagua rais badala ya bunge.

Wafuatiliaji wa siasa za Uturuki wanasema kuwa pendekezo hilo litampa nafasi nzuri zaidi Gul kushinda kwani anaungwa mkono na wananchi wengi.

Waandamanaji hao wana wasi wasi kuwa kuchaguliwa kwa bwana Gul huenda kukapelekea kuanzishwa kwa sheria za kiislam katika nchi hiyo isiyoegemea upande wa dini.