ISLAMABAD.Maandamano bado yaendelea | Habari za Ulimwengu | DW | 26.03.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

ISLAMABAD.Maandamano bado yaendelea

Wafuasi wa upinzani nchini Pakistan wamekuwa wakiendeleza maandamano kupinga hatua ya rais Parves Musharaf ya kumng’oa madarakani jaji mkuu Iftikhar Mohamed Chaudry.

Kabla ya maandamano hayo polisi waliwakamata mamia ya watu kutoka sehemu mbali mbali za nchi hiyo.

Wengi kati ya watu waliokamatwa na kuzuiliwa ni wafuasi wa chama cha Pakistan Peoples na Shirikisho la Waislamu nchini Pakistan.

Makundi yote mawili awali yaliongozwa na waziri mkuu wa zamani anaeishi uhamishoni.

Pakistan tayari imemuapisha jaji mkuu mpya Rana Bhangwandas atakae liongoza jopo la majaji linalotrajiwa kusikiliza kesi dhidi ya jaji aliyetimuliwa Iftikhar Mohamed Chaudry kuanzia April 3.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com