ISLAMABAD:Bhutto atolewa vitisho vingine
24 Oktoba 2007Matangazo
Kiongozi wa upinzani nchini Pakistan bibi Benazir Bhutto ametolewa vitisho vingine juu ya kumwuua, siku chache tu baada ya kufanyika jaribio la kumwuua ambapo watu karibu 140 waliangamia.
Bibi Bhuto amesema atasonga mbele na kampeni yake ya uchaguzi licha ya vitisho hivyo.Walakini mwanasiasa huyo ataepuka mikutano ya hadhara.
Uchaguzi wa bunge umepangwa kufanyika mwezi januari nchini Pakistan.