Iraq karibu kuwakomoa waasi-Al-Malik | Habari za Ulimwengu | DW | 26.01.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Iraq karibu kuwakomoa waasi-Al-Malik

KARBALA:

Waziri mkuu wa Iraq Nuri al-Maliki anasema kuwa vikosi vyake vya usalama vimeanza kile alichokiita hujuma muhimu na za mwisho dhidi ya al Qaeda. Akizungumza katika mji wa Karbala,amesema kuwa vikosi vya Iraq sasa vinaelekea mji wa kaskazini wa Mosul ili kukabiliana na ngome ya mwisho ya waasi wa kisunni.Serikali ya Iraq inalilaumu kundi la Al Qaida kwa mlipuko mkubwa uliotokea mjini Mosul siku ya jumatano ambao uliwauwa watu wasiopungua 35 na kuwajeruhi wengine 200.Jeshi la Marekani linasema kuwa mtandao wa ugaidi umejikusanya katika mikoa ya kaskazini mwa nchi hiyo baada ya kufurushwa kutoka Baghdad na mkoa wa Anbar magharibi.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com