IISS yatoa ripoti ya mwaka | Matukio ya Kisiasa | DW | 10.02.2016
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

IISS yatoa ripoti ya mwaka

Taasisi ya Kimataifa ya masuala ya kijeshi IISS imetoa ripoti yake ya mwaka kuhusu mtazamo wa kijeshi duniani, ikisema ukubwa wa nchi za magharibi panapohusaika na teknolojia ya kijeshi unafifia

MQ-9 Reaper Drohne Drohnenkrieg Ziel Drohnenangriff Afghanistan

Ndege inayoruka bila rubani chapa MQ-9 Reaper

Ripoti hiyo inasema kutokana na kuzidi kupatikana njia za kupata teknolojia kirahisi, dunia inakabiliwa na uwiano wa ngzuvu za kijeshi wenye utata. Sudi Mnette anataarifa kamili kuhusu ripoti hiyo.

Ripoti ya taasisi ya kimataifa ya masuala ya kijeshi pia imeeleza kwamba Urusi na China zimo katika jitihada ya kuboresha majeshi yao na ziko katika harakati za kutengeneza uwezo wao wa kisasa katika sekta hiyo.

Nguvu ya mataifa ya magharibi

John Chipman IISS

Mkurugenzi Mtendaji wa IISS John Chipman

Mkurugenzi mtendaji wa taasisi hiyo ya IISS John Chipman aliliambia Shirika la habari la Ufaransa AFP kwamba Ilikuwa ikifikiriwa kwamba mataifa ya magharibi yalikuwa mabingwa wa teknolojia mpya na yakiongoza katika sekta ya teknolojia dhidi ya mataifa shindani au makampuni yasio ya kitaifa.

Chipman amesisitiza kwamba nguvu za kijeshi katika karne ya 21 hazihusiani tu na kuwa na ndege , vifaru au manowari lakini pia kuwa na teknolojia kama usalama wa mitandao na silaha zinazotumika kwa njia vya mitandano kama vile ndege zisizo na rubani (drones) ambazo huendeshwa kutokea kituo maalum cha nchi kavu.

Kupungua kwa bajeti ya ulinzi

Pia ripoti imesema bajeti za ulinzi za mataifa ya Ulaya ambayo zimepunguzwa sana tokea kuanguka kwa ukuta wa Berlin 1989, bado ni ndogo mno . Mwaka uliopita , ni wanachama wanne tu kati ya 26 wa ulaya katika Jumuiya ya kujihami ya NATO ambao waliweza kufikia lengo la kwamba mbili asilimia ya pato jumla la taifa itumike katika bajeti ya ulinzi. Wanachama hao ni Uingereza, Ugiriki, Poland na Estonia.

Kwa upande mwengine mataifa matano yaliokuwa usoni katika matumizi ya ulinzi mwaka jana ni Marekani dola bilioni 597.5, China dola 145.8 bilioni, Saudi Arabia 81.9 bilioni, Urusi 65.6 Bilioni na uingereza dola 56.2 bilioni. Urusi iliotuma wanajeshi nchini Syria mwezi Septemba imeongeza zaidi matumizi ya ulinzi. Sambamba na hayo kiwango cha matumizi ya kijeshi ya Marekani barani ulaya yameongezwa mara nne kufikia dola bilioni 3.4

Katika kanda ya mashariki ya kati, kuondolewa vikwazo dhidi ya Iran mwaka jana baada ya kupatikana makubaliano kuhusu mpango wake wa Nyuklia, unaongeza uwezekano wan chi hiyo kuboresha zana zake za kijeshi, ambapo sehemu kubwa ni za tokea miaka ya 1970. Mataifa ya Ghuba ambvyo yanatambua kwamba wakati wote Iran itakuwa mbele kwa kiwango cha nguvu za kijeshi, huenda yakajaribu kupata silaha za kisasa kama makombora ya Cruisse, silaha zitakazoyawezesha kushiriki katika harakati za kijeshi, hata ikiwa kutakuwa na upinzani kutoka Iran.

Mwandishi: Sudi Mnette,afp
'Mhariri. Mohammed Abdul-Rahman

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com