IEBC na Safaricom zatoa vielelezo kwa CORD | Uchaguzi Mkuu wa Kenya 2013 | DW | 13.03.2013
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Uchaguzi Mkuu wa Kenya 2013

IEBC na Safaricom zatoa vielelezo kwa CORD

Tume huru ya Uchaguzi na Mipaka nchini Kenya IEBC na kampuni ya simu Safaricom zimekubali kuukabidhi mrengo wa CORD unaoongozwa na Waziri Mkuu Raila Odinga, takwimu za matokeo ya kura ya urais yaliyozua utata.

(130309) -- NAIROBI, March 9, 2013 () -- Kenya's Independent Electoral and Boundaries Commission (IEBC) chairman Issack Hassan addresses the press at the national tallying center in Nairobi, capital of Kenya, March 8, 2013. Kenya's Jubilee Alliance's presidential candidate Uhuru Kenyatta has secured 50.03 percent of votes in general elections, provisional results on early Saturday shows. (/Meng Chenguang)

Tume huru ya uchaguzi na mipaka

Wakati huo huo Mrengo wa Jubilee unaoongozwa Rais Mteule Uhuru Kenyatta nao pia umetaka kukabidhiwa takwimu hizo.

Mawakili wa mrengo wa CORD waliwasilisha ombi hilo mahakamani baada ya Tume ya IEBC kukataa kuwapa nakala za fomu za matokeo ya urais ili waweze kuwasilisha kesi ya kupinga kutangazwa kwa Uhuru Kenyatta kama mshindi wakidai uchaguzi ulikumbwa na hitilafu nyingi. Sikiliza taarifa ya Alfred Kiti kutoka Kenya kwa kubonyeza alama ya masikioni hapo chini.

Mwandishi Alfred Kiti
Mhariri Mohammed Khelef

Sauti na Vidio Kuhusu Mada

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com