Hujuma katika timu ya Mercedes F1? | Michezo | DW | 02.05.2016
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Michezo

Hujuma katika timu ya Mercedes F1?

Dereva Nico Rosberg anaendelea kupata ushindi na Lewis Hamilton akikumbwa na matatizo licha ya kumaliza katika nafasi ya pili katika mashindano ya Jumapili ya Russian Grand Prix

Rosberg alipata ushindi wake wa saba mfululizo na kuutanua uongozi wake wa ubingwa wa dunia kwa pengo la pointi 43. Muingereza Hamilton aliendelea kukumbwa na hitilafu za kimitambo na hajashinda mashindano yoyote msimu huu tangu aliposhinda taji la ulimwengu Oktoba 2015.

Mercedes imepuuza madai kuwa wanampendelea Mjerumani Rosberg kumliko Hamilton msimu huu. Mkuu wa timu ya Mercedes Toto Wolff alisisitiza kuwa hawawezi kamwe kumhujumu Hamilton. Kimi Raikkonen wa Ferrari alimaliza wa tatu katika mashindano hayo ya Sochi nchini Urusi.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/DPA
Mhariri: Yusuf Saumu

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com