1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

HONGKONG:Tung Chee Wah huenda amejiuzulu

7 Machi 2005
https://p.dw.com/p/CFYy

Kiongozi wa Hong Kong amefanya mkutano wa dharura na mrithi mtarajiwa wa mamlaka yake baada ya kuhudhuria mazungumzo huko Beijing.

Duru zimearifu kuwa Tung Chee Wah amejiuzulu mamlaka na kuwa uamuzi wake umekubaliwa na wakuu wake wa China. Hata hivyo Tung amesema kwamba taarifa ya kujiuzulu kwake itatolewa katika wakati unaofaa. Hatua hiyo imeitumbukiza Hongkong kwenye homa ya uvumi wa kisiasa na kutikisa masoko yake muhimu ya kifedha.

Watu wengi wa Hong Kong wameingiwa na wasiwasi kwamba China inajishughulisha zaidi na masuala ya Jimbo hilo licha ya kuahidi kuepuka masuala ya Hong Kong baada ya kumalizika kwa utawala wa kikoloni wa Uingereza.