Hiddink: Conte ana kibarua cha kuijenga upya Chelsea | Michezo | DW | 09.04.2016
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Hiddink: Conte ana kibarua cha kuijenga upya Chelsea

Muitaliano Antonio Conte anakabiliwa na kazi kubwa wakati akichukua mikoba katika klabu ya Cheslea msimu ujao. Hayo ni maneno ya kaimu kocha wa Guus Hiddink.

Kocha wa zamani wa Jubentus Conte ametangazwa kuwa mrithi wa Hiddink na ataanza enzi mpya uwanjani Stamford Bridge baada ya kuiongoza Italia katika dimba la Mataifa ya Ulaya nchini Ufaransa mwezi Juni.

Kazi yake itakuwa ni kuwarejesha mabingwa hao wa msimu uliopita kileleni mwa Premier League baada ya kuwa na msimu mbovu. Hiddink anahisi kuwa kikosi hicho cha Chelsea inakosa wachezaji ambao wanaweza kutegemewa katika kutoa mwongozo wa mafanikio kama ilivyokuwa katika muongo mmoja uliopita.

Hiddink alikutana na Conte Jumatatu wiki hii baada ya kocha huyo mtarajiwa kuzuru uwanja wa mazoezi wa Chelsea ili kujifahamisha na mazingira yake mapya.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/AP/Reuters/DPA
Mhariri: Sessanga Iddi