1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hertha, yapania kurejea kwa kishindo msimu ujao

9 Julai 2020

Klabu ya kandanda ya Hertha Berlin inalenga kurejea katika ligi kuu ya soka ya Bundesliga msimu ujao tofauti na harakati zake katika msimu uliopita, amenukuliuwa akisema Rais wa klabu hiyo, Werner Gegenbauer.

https://p.dw.com/p/3f3tB
Fußball Bundesliga | Hertha BSC - FC Augsburg
Picha: Getty Images/Pool/H. Hanschke

Klabu ya kandanda ya Hertha Berlin inalenga kurejea katika kandanda la Ulaya kwa kufanya vyema katika ligi kuu ya soka ya Bundesliga msimu ujao tofauti na harakati zake katika msimu uliopita, amenukuliuwa akisema Rais wa klabu hiyo, Werner Gegenbauer, wakati akizunguma na gazeti la Bild.

Hertha ilimaliza msimu katika nafasi ya 10 kwenye msimamo wa ligi kuu ya Bundesliga iliyofikia tamati mwishoni mwa mwezi uliopita, huku ikikutana na changamoto nyingi ikiwemo fukuza fukuza ya makocha wanne tofauti katika msimu mzima akiwemo Juergen Klinsmann.

"Tunaangazia mbele, nafasi za juu katika msimamo wa ligi ni malengo yetu. Hii pia inajumuisha kufuzu nafasi ya kucheza michuano ya soka ya Ulaya, bora katika ligi ya Mabingwa,”aliongeza, Gegenbauer

Hertha ambao mnamo mwaka 1978 hadi 1979 walifanikiwa kuingia hatua ya nusu fainali ya kombe la UEFA na mara ya mwisho kwa klabu hiyo kushiriki katika ligi ya Europa ambapo waliondolewa katika hatua ya makundi.

Hertha wanarejea tena katika msimu ujao wa Bundesliga na mfadhiri wao Lars Windhorst ambaye hivi karibuni, alitangaza atawekeza euro milioni 150 sawa dola za Kimarekani 169 kwa klabu hiyo akitaka kuifanya kuwa miongoni mwa miamba ya soka nchini Ujerumani kwa muda mrefu.