HAVANA: Cuba yamuomboleza Vilma Espin | Habari za Ulimwengu | DW | 19.06.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

HAVANA: Cuba yamuomboleza Vilma Espin

Mke wa kaimu rais wa Cuba wa hivi sasa,amefariki dunia mjini Havana akiwa na umri wa miaka 77.Vilma Espin Guillois,alikuwa mpiganaji wa chini kwa chini na alichukua nafasi muhimu katika mapinduzi ya Cuba,yaliyokuja kumweka madarakani shemeji yake Fidel Castro.Tangazo rasmi la kifo chake kwenye televisheni ya taifa,limemsifu kama shujaa wa mapigano ya chini kwa chini,alienawiri katika jeshi la waasi na hakuacha kupigania haki za wanawake na watoto.“Serikali ya Cuba imetangaza kipindi rasmi cha maombolezo hadi leo jioni.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com