Havana. Castro bado mgonjwa. | Habari za Ulimwengu | DW | 23.12.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Havana. Castro bado mgonjwa.

Kiongozi wa Cuba Fidel Castro ambaye ni mgonjwa amekosa kuhudhuria kikao cha mwisho katika mwaka huu cha bunge la taifa, ikiwa ni ishara kuwa utawala wake wa karibu nusu karne nchini Cuba unaweza kuwa unakaribia kwisha.

Kiti ambacho kwa kawaida kinakaliwa na kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 80 katika jengo la mikutano la Havana kilikuwa tupu katika mkutano huo, ambao uliongozwa na mdogo wake wa kiume Raul Castro na wajumbe wengine wa uongozi wa kisiwa hicho wa chama cha kikmunist.

Castro hajaonekana hadharani tangu Julai mwaka huu.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com