Havana. Castro aonekana hadharani tena. | Habari za Ulimwengu | DW | 29.10.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Havana. Castro aonekana hadharani tena.

Kiongozi wa Cuba Fidel Castro ambaye bado anaendelea kuugua amejitokeza hadharani kwa mara ya kwanza baada ya kutoonekana kwa zaidi ya mwezi mmoja, akitembea na kuondoa minong’ono ya hivi karibuni kuwa amefariki katika video iliyotangazwa hewani na televisheni ya taifa.

Castro ambaye amejiuzulu uongozi kwa muda Julai mwaka huu kufuatia upasuaji wa tumbo, hajaonekana tangu katikati ya mwezi Septemba, wakati picha zilizoonyeshwa akiwapokea viongozi wa dunia mjini Havana zilipotolewa.

Kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 80 amesema kuwa hali yake itachukua muda mrefu kurejea kawaida na inaweza kuwa na matatizo, lakini amesema kuwa anapata nafuu kama ilivyopangwa.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com